TAARIFA YA BODI YA WAKURUGENZI YA CPB KWA WAUZAJI WA MAZAO

TAARIFA YA BODI YA WAKURUGENZI YA CPB KWA WAUZAJI WA MAZAO TAARIFA YA BODI YA WAKURUGENZI YA CPB KWA WAUZAJI WA MAZAO Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB), imekuwa katika zoezi la ununuzi wa mazao kwa kipindi cha kuanzia Juni, 2023 hadi sasa, zoezi ambalo linaendelea  katika vituo mbalimbali vya manunuzi vya Bodi Nchi nzima huku malengo yakiwa ni kununua Jumla ya Tani laki moja (100,000) za Nafaka na Mazao mengine Mchanganyiko. Bodi ya Wakurugenzi inawataarifu wauzaji wote wa mazao kuwa malipo yote yatafanyika ndani ya siku tano (5) za kazi kuanzia Jumatatu ya tarehe 21.08.2023 kadiri ununuzi utakavyoendelea. Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Wauzaji,Wakulima na Wadau wetu wote na kuomba ushirikiano wenu katika Kipindi hiki cha manunuzi ya mazao  kwa siku zijazo. "CPB, SULUHISHO LA NAFAKA", Salum Awadh Hagan, Mwenyekiti - Bodi ya Wakurugenzi, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko, Imetolewa Tarehe 18/08/2023.