CPB Kanda ya Kati inajumuisha maeneo ya Dodoma, Singida, Tabora, Katavi na Kigoma. CPB ilipata ardhi manispaa ya Dodoma katika eneo la mbugani barabara ya Veta na  eneo  la Kizota (eneo la viwanda magharibi), yenye wastani wa hekta 3.7 na 1.92 mtawalia.

Ofisi kuu kanda ya kati ipo Kizota, yenye ofisi ndogo – kituo cha mauzo (POS) katika Eneo la Mbugani karibu na majengo ya bunge, ambapo mauzo na manunuzi wa mazao yanashughulikiwa.

Ofisi ya Kanda ya Kati eneo la Kizota ina kiwanda cha kisasa cha kusaga mahindi chenye uwezo wa kusindika tani 60 za mahindi kwa siku, kituo cha kusindika mafuta ya alizeti chenye uwezo wa kusindika tani 20 za alizeti kwa siku, maabara yenye vifaa vya kisasa yenye uwezo wa kufanya kazi kwa ubora ambayo huchunguza bidhaa zinazozalishwa kabla ya kupelekwa sokoni, na kantini ambayo hutoa huduma za upishi kwa jumuiya ya CPB na umma kwa ujumla.

Kanda ya kati pia ina maghala na vifaa vya kuhifadhi nafaka vyenye uwezo wa jumla ya metriki tani 32,000. Maghala yake ya vitanda yanapatikana katika vitengo sita vya tani 5,000 na kitengo kimoja cha tani 2,000. Maeneo hayo ya kuhifadhia yapo mita 300 kutoka kituo cha treni cha Dodoma na mita 200 kutoka barabara kuu ya Dodoma - Dar Es Salaam. Sehemu kituo kilipo pamoja na barabara za lami zinazozunguka kituo hiki huwezesha kwa wingi usafiri wa kwenda na kurudi, hivyo kufanya kufanya hupatikanaji na hufikiaji wa kituo hiki kuwa rahisi. Kituo pia kina nafasi kubwa ya maegesho

BIDHAA NA HUDUMA ZITOLEWAZO

Sisi ni wasambazaji wa bidhaa za kilimo, mbichi na zilizosindikwa. Tunanunua, tunaweka daraja la ubora pamoja na kuuza aina mbalimbali za mazao kama vile mahindi, maharage ya kila aina, mtama, mpunga, karanga na mazao mengine kadri inavyohitajika. Bidhaa zetu zilizosindikwa, ambazo ni pamoja na Dona bora na Sembe bora, mafuta ya alizeti ya CPB yanauzwa kwa jina la chapa NGUVU. Korosho zetu, zilizokaangwa na mbichi zinauzwa kwa jina la chapa Tan Korosho.

Pia tunauza vyakula vya mifugo kama pumba za mahindi, alizeti na mashudu ya pamba. Wilaya za Manyoni, Mpwapwa, Kongwa, Bahi, Chamwino, Chemba, Kondoa, Gairo Singida, Iramba, Itigi, Morogoro, Dar es Salaam na pamoja na wilaya za ukanda wa pwani zinahudumiwa na wasambazaji wetu.

Huduma Zetu Nyingine ni Pamoja na:

Huduma za ushauri kwenye tasnia ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko
Tuna wafanyakazi wenye ujuzi na uzoefu katika tasnia ya nafaka na mazao mchanganyiko, waliobobea katika usimamizi baada ya mavuno, uhifadhi wa bidhaa, usindikaji wa chakula kitaalamu, usimamizi wa mnyororo wa thamani, na uuzaji ndani na nje ya nchi.

 

Kusafisha na kukausha Nafaka na Nafaka na Mbegu za mafuta
Kituo hiki kina mashine za kisasa zenye uwezo wa kusafisha na kukausha tani 60 za nafaka na mbegu zingine zinazohusiana na mafuta kwa siku. Kituo hiki pia kina chumba maalumu ambapo nafaka na mazao mengine yenye unyevu mwingi yanaweza kupunguzwa na kufikia viwango vinavyohitajika

 

Kupima uzito
Ufungaji wa mzani-daraja wa kisasa ambao hutoa usahihi wa juu kwa mizigo mikubwa sasa unaendelea ili kuhudumia kiwanda  na umma kwa ujumla.

 

Kukoboa na kusaga Nafaka
Mashine za kusaga mahindi za kiteknolojia ya Ulaya zilizowekwa Dodoma hutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu zinazofaa kwa matumizi ya binadamu, na teknolojia hii ni rafiki kwa mazingira.

 

Upangaji na Ufungaji wa Nafaka
Baada ya kusafisha, kituo chetu hutoa chaguzi za kupanga na kufunga nafaka kwenye mifuko ya kilo 25, 50, au 100.

 

Huduma za Kujitegemea za Usagishaji kwa Umma
Tunatoa huduma huru za usagaji kwa umma wote kwa bei nzuri na bidhaa za ubora wa hali ya juu zinazokidhi mahitaji ya wateja wetu.

 

Huduma za upishi
Tunatoa huduma za upishi kwa shughuli mbalimbali kuanzia milo ya kila siku hadi milo ya shughuli kama vile mikutano ya bodi, makongamano pamoja na harusi

 

Fursa za kushirikiana na CPB kanda ya kati

  • Uwekezaji katika vifaa vya usindikaji na uhifadhi.
  • Biashara ya bidhaa za kilimo.
  • Wasafirishaji.
  • Usambazaji wa bidhaa za CPB
  • Mawakala wa bidhaa zetu
  • Wakala wa usambazaji na kusafisha
  • Usambazaji wa vifungashio
  • Huduma za uchapishaji,
  • Matangazo na mawakala wa matangazo.
"Tunawaalika wadau wenye uwezo kufanya kazi na Bodi ya Nafaka na Mazao mengine Tanzania"