Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (Cereals and Other Produce Board – CPB) ilianzishwa kwa Sheria ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko Na. 19 ya mwaka 2009 (The Cereals and Other Produce Act No.19 of 2009). Tofauti na Bodi nyingine za mazao ambazo huwa na jukumu la kusimamia zao/ mazao, Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko imepewa jukumu la kufanya biashara ya nafaka na mazao mengine ili kumwezesha mkulima kupata soko la uhakika na bei shindani ya mazao yake.