KANDA YA KASKAZINI (CPB ARUSHA).

Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Kanda ya Kaskazini ilianzishwa mwaka 2019 na  kukabidhiwa rasmi Kiwanda  09/06/2019.

Toka wakati huo CPB Kaskazini  imeendelea kutekeleza majukumu yake ya kufanya biashara ya nafaka na mazao mengine ili kumwezesha mkulima kupata soko la uhakika na bei shindani ya mazao yake.

Kanda ya Kaskazini inaundwa na Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Tanga. Ofisi za Kanda zipo Arusha, Barabara ya Viwandani-Unga Limited.

Kwa sasa Kanda hii iko chini ya Meneja Peter Daniel Mobe ambapo katika kutekeleza majukumu yake, CPB Kanda ya Kaskazini imekuwa inajishughulisha na shughuli zifuatazo:-

1. Ununzi wa Mazao:

CPB Kanda ya Kaskazini imekuwa ikijihusisha na ununuzi wa mazao ya nafaka kama vile Mahindi, Ngano, Mchale na Mtama, aidha imekuwa ikijihusisha na mazao ya jamii ya mikunde kama Maharage na Mbaazi.

2.Uchakataji wa mahindi na ngano:

CPB Kanda ya Kaskazini in kiwanda cha kuchakata (kusaga) unga wa mahindi chenye uwezo wa kuchakata tani 60 za mahindi kwa na kiwanda cha kusaga ngano chenye uwezo wa kuchakata tani 120 za ngano kwa siku.

CPB Kanda ya Kaskazini inatoa huduma ya usagishaji (milling service) kwa Wadau wenye uhitaji wa huduma hiyo.

3. Uuzaji wa bidhaa:

Kanda ya Kaskazini inauza bidhaa mbalimbali ikiwemo mahindi, unga wa wa mahindi (NGUVU Sembe na NGUVU Dona), Unga wa Ngano NGUVU, mafuta ya Alizeti ya NGUVU, Mchele wa NGUVU, Tan Korosho na bidhaa za jamii ya mikunde.

4. Ukaushaji wa Mazao ya nafaka:

CPB Kanda ya Kaskazini inatoa huduma ya ukaushaji wa nafaka kwa Wadau mbalimbali. CPB Kanda ya Kaskazini in mitambo yenye uwezo wa kukausha nafaka kufikia kiwango cha unyenyevu kinachotakiwa kuhidhi.

5. Uhifadhi na Usafishaji wa Mazao:

CPB Arusha inayo miundombinu ya Vihenge yenye uwezo wa kuhifadhi tani 28,800 na ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 10,000 ya mazao. CPB Kanda ya Kaskazini inatoa huduma ya uhifadhi kwa Wadau wenye kuhitaji huduma hiyo.

6. Huduma ya Upimaji wa Magari:

CPB Kanda ya Kaskazini ina mzani mkubwa wenye uwezo wa kupima tani 60. Kanda ya Kaskazini inatoa huduma ya upimaji kwa Wadau mbalimbali wanaohitaji huduma hii.

7. Kilimo cha Mkataba:

CPB Kanda ya Kaskazini imekuwa ikihamasisha kilimo cha Mkataba kwa zao la ngano ili kusaidia upatikanaji wa malighafi ya kiwanda cha unga wa ngano, hivyo watu binafsi na vyama vya Ushirika waliingia mkataba na CPB Kanda ya Kaskazini katika Wilaya za Hanang, Karatu, Monduli na Siha katika msimu wa kilimo 2020/2021, na kiasi cha mbegu tani 210 kilisambazwa na kupandwa kwenye ekari zipatazo 2,937.

Shughuli za Kimasoko:

Mbali na majukumu hayo ya msingi, Kanda ya Kaskazini kupitia kitengo chake cha Masoko na Mauzo imekuwa ikitekeleza shughuli mbalimbali zinazohusu masoko kwani ni muhimu kwa CPB na bidhaa zinazozalishwa kujulikana katika soko ili CPB iweze kufanya mauzo. Kanda ya Kaskazini imekuwa ikishiriki katika maonesho mbalimbali yanayofanyika hapa Nchini kama vile maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba, maonesho ya sikukuu ya Wakulima yaani 88 na maonesho mengine kadri yanavyokuwa yameandaliwa.

Katika msimu wa 2023/2024 Kanda ya Kaskazini tumejipanga kununua mahindi takribani tani 20,000 na Ngano ipatayo tani 27,000 ili viwanda vyetu viweze kufanya kazi kulingana na uwezo wake pamoja na kufanya biashara ya nafaka (trading).

Hivyo tunawakaribisha vyama vya Ushirika(AMCOS), Wakulima wakubwa na wadogo kwa ajili ya kutuletea mazao maana CPB-Arusha ni soko na suluhisho la nafaka.