CPB  ina jukumu la kununua Nafaka na Mazao Mengine kwa ajili ya biashara. Nafaka hizo hununuliwa kupitia Kanda mbalimbali za CPB  katika maeneo yaliyobainika kuwa na uzalishaji mkubwa  wa nafaka.Bodi inafanya jukumu hili kwa kuingia mikataba ya ukulima wa mazao mbalimbali na mikataba ya ununuzi na wakulima ambapo husisitiza katika bidhaa zenye ubora. Bei ambayo hutumika katika mikataba hiyo,ni ile inayotokana na kuangalia gharama za uzalishaji za mkulima na bodi.