Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko imepewa mamlaka ya kufanya biashara katika masoko ya ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu.

CPB imeanzisha vituo vya mauzo katika mikoa mbalimbali ndani na nje ya nchi, ili kuweza kununua bidhaa za CPB ukiwa Tanzania unaweza kutembelea vituo vyetu vya mauzo vilivyopo Dodoma, Arusha, Iringa, Mwanza na Dar es Salaam au unaweza kufanya mawasiliano kupitia simu namba na barua pepe zinazoonekana kwenye tovuti yetu. Pia vituo vya mauzo vilivyoanzishwa nje ya nchi  vinapatikana katika nchi za Kenya (Nairobi), Congo DRC (Lubumbashi) na Sudani ya Kusini (Juba), ambapo bidhaa za CPB zinapatikana.

Lengo la CPB ni kuendelea kutumia ubunifu mbalimbali katika kutekeleza miradi ya kimaendeleo ili kupanua soko la nafaka nchini na kuanzisha masoko mapya ya nje ya nchi. 

Hata hivyo ili kuhakikisha bidhaa za CPB zinapata soko kubwa, Bodi imejikita katika kuongeza thamani kwenye bidhaa zake kwa kuzingatia ubora, usafi wa hali ya juu pamoja na kutumia technolojia za kisasa kwenye viwanda katika kuzalisha bidhaa zake.


MAWASILIANO:

NAMBA ZA SIMU:

MAKAO MAKUU DODOMA.
+255(0)677 073 939
+255(0)715 003 590

 

KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI.
+255(0)677 078 404
+255(0)677 078 401

 

KANDA YA ZIWA
+255(0) 677 073 932
+255(0) 677 073 938

 

KANDA YA KASKAZINI.
+255(0)678 033 408
+255(0)677 073 937

 

KANDA YA KATI
+255(0)677 078 403
+255(0)715 073 936

 

KANDA YA MASHARIKI
+255(0)677 078 434
+255(0)752 333 334
+255(0)715 003 590

 

CONGO
NAIROBI
JUBA
BARUA PEPE:
info@cpb.go.tz
sales@cpb.go.tz