KPMG KUANDAA MPANGO MKAKATI WA CPB
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) Ndg: John Damas Maige ameongoza zoezi la utiaji saini kati ya CPB na Kampuni ya KPMG ambao ni wabobezi kwenye eneo la ushauri wa kitaalamu wa biashara (business consultancy) na uandaaji wa mipango mikakati kwaajili ya kuandaa mpango mkakati wa miaka mitano wa Bodi utakaoongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Bodi kwa kipindi hicho.