Ninayo furaha  kuwaalika wadau na wateja wetu wote kwenye tovuti mashuhuri ya CPB ambapo mtaweza kupata taarifa muhimu zinazohusu dhamira yetu, malengo, shughuli na fursa mbalimbali.Natoa wito kwa wadau wote, wakulima, vyama vya ushirika, wafanyabiashara, wasafirishaji, taasisi za fedha, wasambazaji pembejeo za kilimo, wakala binafsi na Serikali n.k kushirikiana nasi katika kuhakikisha kuwa kilimo biashara kinachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi na kuleta tija kwa watu wa Tanzania, Afrika na Dunia kwa ujumla.
Dira yetu ni kuwa Shirika kubwa  la kibiashara ya  mazao ya kilimo lenye uwezo wa kuzalisha, kusindika, kusambaza na kuuza Bidhaa za kilimo zenye ubora wa juu barani Afrika na Duniani kwa ujumla. Tunatarajia kubadili maisha ya watu nchini Tanzania, Afrika na duniani kwa kuleta ubunifu katika kutengeneza nafasi za kazi, kutumia fursa za kibiashara na kubadilishana maarifa na ujuzi. Shirika linatazamia kushirikiana na wafanyabiashara makini na wawekezaji kwa lengo la kuimarisha uwezo na hatimaye Shirika kufikia malengo yake.
Moto wetu ni kutafuta masoko kwa Wakulima wa Tanzania, Barani Afrika na kwingineko, Kuweka uwezo thabiti wa usambazaji wa bidhaa katika miji yote  nchini Tanzania, miji ya kimkakati barani Afrika na kwingineko.
Ushindani katika masoko utakuwa thabiti  kupitia kilimo cha mkataba ambapo wakulima wadogo wanapewa kandarasi hasa kupitia vyama vya ushirika na kusaidiwa na huduma za ugani, pembejeo za kilimo na huduma za bima ya mazao. Hii itahakikisha mavuno ya juu na yenye ubora  yanapatikana ili kukidhi mahitaji ya ubora na bei pinzani katika soko la kimataifa. Zaidi ya hayo, soko endelevu la mazao ya wakulima linapatikana kwa kuanzisha na kuendesha kwa ufanisi viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na hifadhi katika maeneo ya kimkakati nchini Tanzania.
Kwa kuzingatia  sharti la hapo juu, tunakuwa na  matokeo dhabiti yenye mwelekeo, wafanyakazi wenye uwezo mkubwa na utamaduni wa biashara  ulio na uadilifu, kufanya kazi kwa pamoja, kujitolea na kufanya kazi kwa bidii kupitia kuajiri wafanyakazi makini, kufundisha, kuhamasisha, mafunzo ya mara kwa mara kwakushirikiana na makampuni  ya ndani na nje ya nchi.
Patrick Mongella, Mkurugenzi Mkuu.
Inawezekana, inaweza kufanyika, tuweke nia  na akili zetu kwa pamoja!